1
SAUTI ya Yesu niliisikia, Kwa pendo aliniambia: ‘‘Ufike, nataka kukusaidia, Nangoja, nangoja, ufike!’’
Kiitikio
Njoo kwa Yesu, ufike upesi, Uupokee wokovu wa Mungu! Mbona kukawa dhambini, rafiki? Yesu anakuita, njoo!
2
Ukiwa na hofu kufika kwa Yesu, Uliye na dhambi rohoni, Kumbuka ya kuwa huruma ni tele; Ufike kwa Yesu, angoja!
3
Ukiwa maskini, dhaifu kabisa, Mwokozi anakufahamu. Anakuambia: ‘‘Pokea neema, Uache mzigo wa dhambi!’’
4
Na kama nilivyo ninamfikia Mwokozi aliyenipenda. Ninaupokea wokovu na raha; Kwa shangwe ninamshukuru!
