1
PIGA makengele ya furaha leo Kwa sababu mtu ametubu! Mwana mpotevu amerudi sasa, Baba amemsamehe yote.
Kiitikio
Nyimbo za furaha ya mbinguni, Nyimbo za furaha za wakristo! Tuna’sifu Mungu kwa sababu sasa Mtu huyu amwamini Yesu.
2
Piga makengele, ni furaha nyingi; Mkosaji amefunguliwa! Yesu alivunja minyororo yake, Alimpa roho ya kimwana.
3
Piga makengele! Hiyo ni habari Ya kupasha mbali na karibu. Mtu amepata kuwa mtu mpya, Dhambi zake zimeondolewa!
