1
TUNASIKIA leo habari, Inawaita watu wafike; Watu wa hapa, watu wa mbali, Wote wapate sasa wokovu!
2
Mtu wa dhambi, uje upesi, Yesu angoja kukuokoa! Tena kwa nini unachelewa? Leo ni siku ya kuokoka.
3
Ulikimbia Yesu Mwokozi Aliyekukomboa kwa damu. Usikimbie mbali zaidi, Ila urudi, uje upesi!
4
Katika dhambi hutaiona Raha halisi, hata kidogo. Yesu mwenyewe atakujaza Raha ya kweli ndani ya roho.
5
Mtu wa heri katika shida, Katika mambo yote ya huku, Ni hali ya mkristo wa kweli, Mtu wa heri hata milele.
