SASA TAYARI KWETU SIKU YA KUOKOKA

1

SASA tayari kwetu Siku ya kuokoka, Yesu alitimiza Yote msalabani. Wengi wanamjia Yesu Mwokozi wao, Wapate kustarehe, Wapone nafsi zao.

Kiitikio

Mwana-Kondo’ wa Mungu Tunakusifu sana! Uzima uliweka Kwa ’jili yetu sisi. Umetufanya kuwa Mitume yake Mungu. Kati’ majina yote Lako ni kubwa mno.

2

Wewe kwa damu yako Ulikomboa sisi, Na jua la neema Linatuangazia. Tumefahamu sasa Pendo la Mungu wetu. Damu imetuunga Kati’ agano jipya.

3

Njoo upesi nawe Uliyesitasita! Mungu atakujaza Neema yake kubwa, Raha rohoni mwako Inayokutuliza, Matumaini, nguvu, Pendo lililo bora.