NEEMA YA BWANA NI KUBWA SANA

1

Neema ya Bwana ni kubwa sana, Kubwa kuliko zambi za watu, Kule Kalvari tunaiona, Pa’li pa kufa kwa Bwana Yesu.

Kiitikio

Neema yake inasamehe makosa yetu, Neema yake kubwa kuliko uovu wetu.

2

Tuko katika hatari kubwa, Tutapotea tusipotubu; Neema ya Bwana inaonyesha Yesu Mwokozi ni Kimbilio.

3

Ndugu, huwezi kuficha zambi, Mungu mbinguni anaziona! Ee unataka kusukuliwa? Damu ya Yesu itakuosha.

4

Neema ya Bwana ni kubwa sana, Iko tayari kwawe, mupenzi; Kiri makosa, amini Yesu. Atasamehe kwa neema yake.