MWOKOZI WANGU ALINIMWANGIA DAMU

1

Mwokozi wangu alinimwangia damu yake; Kwa mwenye zambi, mwenye haki alitoa mwili.

Kiitikio

Kule kwa musalaba wa Yesu Mwokozi Niliacha zambi zangu kabisa; Nilimupokea na nimeokoka, Na sasa furaha inazidi.

2

Makosa yangu yalifunga Yesu kwa Kalvari; Huruma na mapendo yake ni makubwa kweli.

3

Na giza lilificha Yesu pale kwa Kalvari : Ajabu kubwa, Mwumba wangu alikufa kwami!

4

Siwezi kulipia deni kwa huzuni yangu, Lakini nitatoa vyote kwa Mwokozi wangu.