NINAKUOMBA, YESU

1

Ninakuomba, Yesu, ndiwe Kondoo wa Mungu, Wewe Mwokozi, Sasa unisikie, vile unisafishe, Unitakase niwe wako pekee.

2

Kwa neema yako kubwa unipe mimi nguvu Kwa kazi yako; Ulinikufilia, hivi mapendo kwawe Yawake ndani yangu kama moto.

3

Dunia ina giza, mateso, na huzuni, Uniongoze; Ee, ufukuze giza, machozi upanguse; Usiniache kukufuata mbali.

4

Siku ya kufa kwangu, ninapokwenda ngambo, Sitaogopa; Mikono ya mapendo itanibeba kwako, Niwe pamoja nawe kwa milele.