TUTAFUFUKA KUSIMAMA

1

Tutafufuka kusimama mbele yake Bwana Yesu; Habari zetu tutatoa kwake kwa matendo yetu.

Kiitikio

Nitaonekana mbele yake, jina langu litaitwa naye; Sita’gopa, ninaamini damu ya Mwokozi Yesu.

2

Nitapokea taji ya uzima mikononi mwake; Nitaitupa mbele yake Yesu anayestahili.

3

Tutakutana kwa milele pale, taabu itakwisha; Mizigo tuta-acha kwa miguu ya Yesu Mukombozi.