1
Watu wa Kristo, angalieni, mwone alama za kuonyesha Kwamba Mwokozi atatokea, ni yeye tunayemungoja na hamu.
Kiitikio
Atarudi hakika, atarudi hakika, Ni Yesu mwenyewe waliyemukana ; Atarudi hakika, atarudi hakika, Mwenye utukufu atarudi hakika.
2
Huko dunia, giza na zambi zinazunguka watu wa Mungu ; Mioyo mizito itageuzwa kupata furaha kwa siku ya Bwana.
3
Kuja, Mupenzi, tunakungoja, hamu ya kukuona ni kubwa ; Tutakutana ndani ya hewa, taraja hii tamu : milele na wewe.
