NINA MWOKOZI ANAYENIOMBEA

1

Nina Mwokozi anayeniombea, Rafiki kuliko wengine wo wote; Na sasa mbinguni ananitunza sana, Laiti upate Mwokozi mwenyewe!

Kiitikio

Ninakuombea, ninakuombea. Ninakuombea, upate kuamini!

2

Nina taraja kutoka Baba wangu, Ya kama atanipokea mbinguni; Na sasa ninamungojea kuni-ita, Laiti upate taraja yenyewe !

3

Nina mavazi yanayoningojea, Mavazi meupe ndiyo utukufu ; Na nitayapata mbinguni kwake Mungu, Laiti upate mavazi yenyewe !

4

Nina salama inayopita yote, Si kama dunia inayoitoa ; Inatoka Yesu kwa pendo lake kubwa, Laiti upate salama yenyewe!