HATUA MOJA INAKUTENGA NA MWOKOZI

1

Hatua moja inakutenga na Mwokozi; Unangoja nini? Ufike kwake leo!

Kiitikio

Hatua moja, hatua moja; kuja, anangoja; Kuja kutubu zambi, atasamehe zote! Usikatae tena wokovu wake Mungu!

2

Hatua moja mbele, anakungoja sasa; Amini Neno lake, na utasamehewa.

3

Hatua moja mbele, uzima utaona ; Siku si nyingi huko, unangojea nini?

4

Hatua moja mbele, kwa nini unakawa? Omba: Ee Bwana Yesu, unipoke-e sasa!