1
Sina akili nyingi kufahamu Neno lake Mungu, Najua hili moja tu : Yesu ni Mwokozi wangu.
2
Najua alikufa kwa Kalvari kwa makosa yangu ; Ninahitaji Yesu tu kuwa Mukombozi wangu.
3
Siwezi mimi vile kufahamu pendo lake kubwa. Na linanishangaza tu, pendo la Mwokozi wangu.
4
Na sasa anaishi kwa pahali pa Mbinguni juu ; Yeye Mufalme wangu tu, ndiye Mukombozi wangu.
