Zaburi 87

Zaburi 87
Sifa Za Yerusalemu
Zaburi ya wana wa Kora. Wimbo.
1 Ameuweka msingi wake katika mlima mtakatifu;
2 Bwana anayapenda malango ya Sayuni
kuliko makao yote ya Yakobo.
3 Mambo matukufu yanasemwa juu yako,
ee mji wa Mungu:
4 “Nitaweka kumbukumbu ya Rahabu*Rahabu hapa ni jina la ushairi la Misri. na Babeli
miongoni mwa wale wanaonikubali mimi:
Ufilisti pia na Tiro, pamoja na Kushi,†Kushi hapa ina maana ya Naili ya juu, yaani Ethiopia.
nami nitasema, ‘Huyu alizaliwa Sayuni.’ ”
 
5 Kuhusu Sayuni itasemwa hivi,
“Huyu na yule walizaliwa humo,
naye Aliye Juu Sana mwenyewe
atamwimarisha.”
6 Bwana ataandika katika orodha ya mataifa:
“Huyu alizaliwa Sayuni.”
7 Watakapokuwa wanapiga vinanda wataimba,
“Chemchemi zangu zote ziko kwako.”

*Zaburi 87:4 Rahabu hapa ni jina la ushairi la Misri.

†Zaburi 87:4 Kushi hapa ina maana ya Naili ya juu, yaani Ethiopia.


Biblica® Toleo Wazi Neno: Bibilia Takatifu™Copyright © 1984, 1989, 2009, 2015 Biblica, Inc.
Scripture text reproduced under Creative Commons Attribution–ShareAlike 4.0. Original Scripture wording is unchanged; navigation and presentation are adapted under the same license. Original edition: Read on eBible.org. Full edition and license information.