Zaburi 120

Zaburi 120
Kuomba Msaada
Wimbo wa kwenda juu.
1 Katika dhiki yangu namwita Bwana,
naye hunijibu.
2 Ee Bwana, uniokoe kutoka midomo ya uongo
na ndimi za udanganyifu.
 
3 Atakufanyia nini,
au akufanyie nini zaidi, ewe ulimi mdanganyifu?
4 Atakuadhibu kwa mishale mikali ya shujaa,
kwa makaa yanayowaka ya mti wa mretemu.
 
5 Ole wangu kwa kuwa naishi Mesheki,
kwamba naishi katikati ya hema za Kedari!
6 Nimeishi muda mrefu mno
miongoni mwa wale wanaochukia amani.
7 Mimi ni mtu wa amani;
lakini ninaposema, wao wanataka vita.

Biblica® Toleo Wazi Neno: Bibilia Takatifu™Copyright © 1984, 1989, 2009, 2015 Biblica, Inc.
Scripture text reproduced under Creative Commons Attribution–ShareAlike 4.0. Original Scripture wording is unchanged; navigation and presentation are adapted under the same license. Original edition: Read on eBible.org. Full edition and license information.