Zaburi 110

Zaburi 110
Bwana Na Mfalme Wake Mteule
Zaburi ya Daudi.
1 Bwana amwambia Bwana wangu:
“Keti mkono wangu wa kuume,
mpaka nitakapowafanya adui zako
kuwa mahali pa kuweka miguu yako.”
 
2 Bwana ataeneza fimbo yako ya utawala yenye nguvu kutoka Sayuni;
utatawala katikati ya adui zako.
3 Askari wako watajitolea kwa hiari
katika siku yako ya vita.
Ukiwa umevikwa fahari takatifu,
kutoka tumbo la mapambazuko
utapokea umande wa ujana wako.*Au: vijana wako watakujia kama umande.
 
4 Bwana ameapa,
naye hatabadilisha mawazo yake:
“Wewe ni kuhani milele,
kwa mfano wa Melkizedeki.”
 
5 Bwana yuko mkono wako wa kuume,
atawaponda wafalme siku ya ghadhabu yake.
6 Atawahukumu mataifa, akilundika mizoga
na kuwaponda watawala wa dunia nzima.
7 Atakunywa maji katika kijito kando ya njia,†Au: Yeye atoaye mtu wa kurithi mwingine atamweka kwenye mamlaka.
kwa hiyo atainua kichwa chake juu.

*Zaburi 110:3 Au: vijana wako watakujia kama umande.

†Zaburi 110:7 Au: Yeye atoaye mtu wa kurithi mwingine atamweka kwenye mamlaka.


Biblica® Toleo Wazi Neno: Bibilia Takatifu™Copyright © 1984, 1989, 2009, 2015 Biblica, Inc.
Scripture text reproduced under Creative Commons Attribution–ShareAlike 4.0. Original Scripture wording is unchanged; navigation and presentation are adapted under the same license. Original edition: Read on eBible.org. Full edition and license information.